ALI KIBA |
Akifunguka jana kupitia kipindi cha “The Jump off” cha Times fm, AD anadai alikutana na Ally kwenye show Mbeya akimtaka wafanye “collabo”, AD alidai alimpa vionjo Ally lakini baada ya miezi kadhaa akashangazwa kuisikia chekecha redioni.
- “Tulikutana Mbeya nikamwambia bro nina Idea kali, sijamtafuta bado ila next week nakuja dar nitamtafuta then taratibu zingine zitafuata” alisema Ahmad
Katika hatua nyingine “The jump off”, ilimtafuta meneja wa kundi linalowajumuisha Ally Kiba na Abdu Kiba( kiba square) Kapasta 4 real, ambaye amedai kwamba huo ni uzushi na jamaa ana lengo la kutafuta umaarufu kupitia mgongo wa Ally Kiba.
- “Ile nyimbo Ally kaandika studio, melody pamoja na kila kitu so huyo jamaa aache ujinga wake,asizingue tutampeleka kwenye viombo vya sharia asichezee kazi za watu” alimaliza Kapasta.
Post a Comment