Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MELI ILIYOKUWA NA WATU ZAIDI YA 450 YAZAMA NCHINI CHINA

Meli ya Dongfangzhixing iliyozama.
Shughuli za uokoaji zikifanyika.
Kikosi cha Uokoaji kikiwa kazini.
Juhudi za uokoaji zikiendelea.
Boti maalum za uokoaji.
Waandishi wa habari wakichukua tukio hilo.
Meli ya uokoaji ikielekea eneo la tukio.
Mmoja wa wahanga wa ajali hiyo akifungwa kamba ili aokolewe kutoka majini.
...akiokolewa.
Meli ya Dongfangzhixing ilivyopata ajali.
Majeruhi katika ajali hiyo akipelekwa kwenye huduma.
Ndugu wa baadhi ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo wakiwa na simanzi.
China
Meli ya Dongfangzhixing ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imepinduka na kuzama baada ya kukumbwa na dhoruba la upepo mkali katika mto Yangtze kusini mwa China.
Taarifa zimeeleza kuwa, meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Mashariki mwa Mji wa Nanjing kwenda Chongqing Kusini Magharibi mwa China ndipo ilipozama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Meli hiyo ya Dongfangzhixing au Nyota ya Mashariki ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa Shirika la Usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Serikali ya China, Xinhua ni kwamba, watu wanane wameokolewa mpaka sasa. Kikosi cha Uokoaji kinaendelea na juhudi za uokoaji kwa abiria wengine ambao hawajapatikana mpaka sasa. Japo kazi ya uokoaji inakwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa zinazonyesha.
Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang amedfika eneo la tukio na kujionea maafa hayo.
Kwa upande wao Nahodha na Mhandisi Mkuu, ambao ni miongoni mwa waliookolewa wamekaririwa wakisema kuwa, meli ilikumbwa na kimbunga kikali ikapinduka na kuzama wakati huohuo.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.
Inasemekana kuwa, waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya Shanghai.
Ikumbukwe kuwa, mwezi Januari watu 22 walifariki dunia kwenye mto huo wakati boti iliyokuwa kwenye majaribio kuzama karibu na Zhangjiagang, katika jimbo la Jiangsu.
NA BBC
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top