Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Rais Wa Msumbiji,Fellipe Jacinto Nyusi Alihutubia Bunge la Tanzania......Aahidi Kuendeleza Ushirikiano

Rais wa Msumbiji Fellipe Jacinto Nyusi jana amelihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alisema ziara yake imelenga kuja kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili tangu enzi za harakati za ukombozi.

Rais Nyusi alisema hayo jana wakati alikilihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu nchini ambapo alisema siku zote maendeleo ya nchi yanatokana na uhusiano mzuri baina ya nchi na nchi.
 
Bw. Nyusi ambaye anakuwa Rais wa kwanza wa Msumbiji kuhutubia bunge la Tanzania, alisema kuwa mbali na ushirikiano mzuri wa kisiasa angependa kuendeleza ushirikiano wa kibiashara, elimu na katika nyanja nyingine mbalimbali.
 
Rais Nyusi ambaye aliingia nchini Juzi ameshafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kisha akaelekea visiwani Zanzibar ambapo alikutana na Rais wa visiwa hivyo Dkt, Ali Mohammed Shein na jana alimalizia ziara yake Bungeni mjini Dodoma.
 
Katika hotuba, Rais Nyusi pia aliahidi kushirikiana na Tanzania katika ulinzi wa amani pamoja na vita dhidi ya ugaidi katika mataifa ya Afrika.
 
Kwa upande wake spika wa bunge la Muungano Mh. Anne Makinda alisema kuwa ni heshima kubwa kwa Rais huyo wa kwanza wa msumbiji kuhutubia bunge na kuongeza wataendelea kukuza uhusiano baina ya nchi hizo ili kuleta maendeleo ya nchi hizo.
 
Makinda alisema kumekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa ambao kwa sasa wataendeleza mshikamano kati ya wabunge wa Tanzania na Msumbuji ili kuboresha maisha ya wananchi wa nchiu zote mbili.
Mpekuzi
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top