Edward Lowasa ameendelea kuvunja rekodi ya idadi ya watu wanaojitokeza kumdhamnini baada ya kupata wadhamini 120,392 jana mkoani Arusha.
Rekodi hiyo ya Arusha imezipiku ile iliyowekwa na mkoa ya Iringa alikodhaminiwa na wanachama 58,562.
Mbunge huyo wa Monduli aliwasili jijini Arusha saa
9:00 alasiri na kupokelewa kwa mbwembwe zilizoambatana na nyimbo
mbalimbali za wasanii kadhaa nchini. Lowassa aliongozana na mkewe Regina
na viongozi kadhaa wa CCM.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Lowassa alifanyiwa maombi
rasmi na wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai, maarufu kama Malwaigwana.
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isaack
Joseph alisema waliomdhamini waziri huyo mkuu wa zamani ni wanachama hai
kutoka wilaya zote saba za kichama mkoani Arusha.
Kwa CCM, mkoa wa Arusha una wilaya za Arusha
Mjini, Karatu, Longido, Monduli, Ngorongoro, Arumeru Mashariki na
Arumeru Magharibi.
Post a Comment