Makamba katika hotuba yake amesema itachukua miaka mingi hata kumi kwa Tanzania kuanza kuvuna gesi na rais ajaye anaweza akaondoka madarakani bado gesi haijaanza kutumika.
Huu ni uongo wa wazi ana pengine inaweza kuwa ni kutojua kwamba tayari gesi imeanza kutumika kwenye maeneo mengi ikiwemo kweye viwanda mbalimbali hususani kwenye jiji la Dar es Salaam na kuna maeneo mengine kwenye majumba inatumika.
Namshangaa Januari anaposema gesi haitotumika kwa miaka ya karibu, anataka kutuambia hata mioundo mbinu ya gesi iliyojengwa itaanza kufanya kazi baada ya miaka kumi?
Namshauri aache kuzungumzia mambo ambayo hayajui na kama anatamani kuyazungumzia basi angeuliza kwa wataalamu wa masuala ya gesi kabla ya kufungua mdomo kuongea asiyoyajua.
Kwa mujibu wa wizara ya nishati na madini gesi itaanza kutumika miezi michache ijayo na tayari mabomba ya gesi yamekamilika kwa asilimia 90 na hata kiwanda cha DANGOTE kinachojengwa kitatumia gesi hiyo ambapo kiwanda hicho kitaanza uzalishaji mwezi wa nane kwa maana hiyo gesi itaanza kutumika kabla ya kiwanda hicho kuanza uzalishaji,
Post a Comment