Mkuu wa Utumishi jeshini, Meja Jenerali Vicent Mritaba alitoa onyo hilo mjibi hapa juzi alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya askari wapya katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa la Oljoro.
“Jeshi halitawavumilia askari wanaovunja sheria kwa kushiriki vitendo vinavyokiuka maadili ikiwamo kujichukulia sheria mkononi,” alisema Meja Jenerali Mritaba.
Alisema jukumu la JWTZ ni kulinda mipaka ya nchi, raia na mali zao na kushiriki kazi za kijamii kulingana na mahitaji ya wakati huo.
Pia aliwaonya askari kutoshiriki wala kujihusisha na makundi maovu kwa sababu itawaondolea sifa ya kuendelea kutumikia jeshi hilo lililoundwa rasmi mwaka 1964, baada ya kuvunjwa jeshi lililorithiwa kutoka kwa wakoloni.
Katika hatua nyingine, Meja Jenerali Mritaba aliwataka wanajeshi wajiepushe na vitendo vinavyoweza kuwasababishia maambuziki ya virusi vya Ukimwi.
“Mlipojiunga jeshini wote mlipimwa afya zenu na kugundulika kuwa mpo salama. Epukeni ngono kwa sababu mkipata maambukizi hayo ndoto zenu za kulitumikia taifa zitakatika lakini pia malengo yenu ya kimaisha yatafifia,” alisema.
Awali, Mkuu wa Mafunzo ya Awali ya kijeshi katika Chuo cha Kihangaiko mkoani Pwani, Kanali Ramadhani Churi alisema licha ya changamoto kadhaa kiutawala, wahitimu hao wamefaulu katika hatua zote mbili za mafunzo kuanzia ya wiki sita ya kuwaondoa kwenye hali ya kawaida kuwa wanajeshi.
Kanali Churi alisema askari hao walifundishwa uvumilivu na kuishi katika mazingira magumu ikiwamo kutolala kwa wiki sita mfululizo, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kisaikolojia wa kuhimili jambo lolote gumu kwenye uwanja wa vita na mapambano.
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha 833KJ Oljoro, Luteni Kanali Sijaona Myala alitaja baadhi ya mambo yaliyofanikisha mafunzo hayo kuwa ni kila mtu kuzingatia taaluma na kutekeleza wajibu wake kuanzia kwa wakufunzi, madaktari na viongozi.
Na udaku specially
Post a Comment