GLADNESS MALLYA
DOKTA Chale ambaye anaandika makala za afya katika
gazeti ndugu la hili la Ijumaa, ameanika chanzo cha mastaa wengi kupata
ugumba ambapo pamoja na vyanzo vingine, ameyataja madawa ya kuongeza
maumbile ya mwili na ya kujichubua yanasababisha tatizo hilo.
Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.
Akizungumzia madawa hayo pasipo kuyataja majina (yamezagaa mitaani),
dokta Chale alisema baadhi ya madawa hayo yana kemikali ambazo hupenya
hadi kwenye figo na kuzisababishia madhara ambapo moja kwa moja hawezi
tena kupata mtoto.
Alisema amekuwa akisikia kila kukicha katika vyombo vya habari mastaa
wakijieleza kuwa wamehangaika sana kupata watoto lakini imeshindikana
pasipo kujua madawa hayo ndiyo chanzo hivyo ni vyema wakachukua
tahadhari.
“Kwa wale ambao bado hawafikirii kuzaa ni vyema wakawa
makini na madawa haya ya kuongeza maumbo yao. Yanaathiri figo na
zikishaathirika mwanamke hawezi tena kupata ujauzito.

“Ni
vyema wakawaona madaktari kwa ajili ya ushauri kabla hawajaanza
kuyatumia maana baadhi ya dawa hizi zinaingizwa nchini bila kukaguliwa
kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu,” alisema Dokta Chale.
Miongoni mwa mastaa ambao wamesharipotiwa kuwa na tatizo la kukosa
watoto kwa muda mrefu ni pamoja na mbunge mtarajiwa, Wema Sepetu
‘Madam,’ Judith Wambura ‘Jide,’ Rehema Chalamila ‘Ray C’ (pichani),
Mainda Suka, Jacqueline Wolper na Jokate Mwegelo ‘Kidoti.’
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;
Filed Under:
Gossip
on Saturday, 20 June 2015
Post a Comment