Staa wa filamu za Nollywood, Omotola Jalade.
Lagos, NigeriaSTAA wa filamu za Nollywood, Omotola Jalade, ameamua kufunguka juu ya maisha anayoishi na mume wake, Matthew Ekeinde.Omotola ambaye hivi karibuni alifanya mkutano na vijana mbalimbali wenye ndoto za kucheza filamu, aliwaeleza juu ya maisha anayoishi na mumewe kuwa, yeye kazi yake kubwa ni kupika tu.
Omotola akiwa na mumewe.
“Mimi kazi yangu kubwa katika maisha yetu ya ndoa ni kupika na mume
wangu huwa anakwenda sokoni na dukani kwa ajili ya kununua mahitaji
mbalimbali,”alisema Omotola.
Mama huyo wa watoto wane, aliongeza: “Huwa siendi kabisa sokoni wala dukani, hiyo ni kazi ya mume wangu, mimi napika tu chakula cha aina yoyote ambacho mume wangu atahitaji.”
Post a Comment