VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vimetangaza mgawanyo wa majimbo 253 kati ya majimbo 265 ya uchaguzi Tanzania Bara huku majimbo 12 yakibaki kwenye majadiliano.
Kwa upande wa Zanzibar majimbo yote ya uchaguzi
wamekabidhiwa Chama cha Wananchi (CUF) isipokuwa Jimbo la Mkwajuni
ambalo wamepewa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano ya pamoja
miongoni mwa vyama vinavyounda umoja huo. UKAWA unaundwa na vyama vinne
vya siasa ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na NLD.
Taarifa ya mgawanyo huo imetolewa leo mchana jijini Dar es Salaam na
Makaimu Katibu Wakuu wa vyama hivyo; Sheweji Mketo (CUF), Nderakindo
Kessy (NCCR – Mageuzi), Masudi Makujunga (NLD) na John Mnyika (Chadema)
na taarifa hiyo kusainiwa kwa mapoja.
Mketo amesema vigezo vilivyotumika katika mgawanyo huo ni chama
kilichoongoza katika matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 katika jimbo
husika, matokeo ya udiwani katika kata za majimbo.
Pia matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014, mtandao
wa vyama katika eneo husika, mila na desturi katika eneo husika, ubora
wa mgombea na maridhiano ya vyama vyote.
“Hii ndiyo taarifa ya kwanza rasmi kuhusu mgawanyo wa majimbo.
Tunasisitiza wanachama wetu wanapaswa kutambua kwamba, taarifa hii
haihusiani na mchakato wa kuwapata wagombea wa udiwani. Tulishatoa
mwongozo kuhusu upatikanaji wa wagombea ngazi ya udiwani,” amesema
Mketo.
Ufuatao ni mgawanyo wa majimbo katika kila mkoa Tanzania Bara;-
Mkoa wa Mara
Kwenye mkoa huu majimbo yote tisa wamekabidhiwa Chadema. Majimbo hayo
ni Rorya, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Musoma Vijijini, Butiama,
Bunda Mjini, Mwibara, Musoma Mjini na Bunda Vijijini.
Mkoa wa Simiyu
Chadema wamegawiwa Jimbo la Bariadi, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Kisesa, Meatu, Itilima ambapo Busega limekwenda kwa CUF.
Mkoa wa Shinyanga
Majimbo ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ni Msalala, Kahama Mjini, Kahama
Vijijini, Shinyanga Mjini, Kishapu na Ushetu yamekwenda Chadema.
Mkoa wa Mwanza
Jimbo la Ukerewe, Magu, Nyamagana, Buchosa, Sengerema, , Ilemela,
Misungwi yamekabidhiwa Chadema kuhu Jimbo la Kwimba na Sumve
wakikabidhiwa CUF.
Mkoa wa Geita
Bukombe, Busanda, Nyang’wale, Chato na Mbogwe yamekwenda Chadema.
Mkoa wa Kagera
Jimbo la Karagwe, Kyerwa, Bukoba Mjini, Muleba Kaskazini, Muleba
Kusini, Biharamulo yamekwenda Chadema ambapo Jimbo la Ngara na Nkenge
yamekwenda NCCR-Mageuzi na Bukoba Vijijini limechukuliwa na CUF.
Mkoa wa Mbeya
Katika Mkoa wa Mbeya Jimbo la Lupa, Songwe, Mbeya Mjini, Kyela,
Rungwe, Busekelo, Mbozi Mashariki, Momba, Mbeya Vijijini, Tunduma na
Viwawa yamekwenda Chadema huku Ileje likikabidhiwa kwa NCCR.
Mkoa wa Iringa
Jimbo la Ismani, Kalenga, Mufindi Kaskazini, Iringa Mjini, Kilolo na
Mafinga Mjini yamekabidhiwa kwa Chadema ambapo Jimbo la Mufindi Kusini
linapiganiwa na NCCR-Mageuzi.
Mkoa wa Dar es Salaam
Jimbo la Ubungo, Kawe, Ukonga, Ilala na Kibamba ni Chadema huku Kinondoni, Temeke, na Mbagala ikielekezwa kwa CUF.
Mkoa wa Njombe
Njombe Kaskazini, Lupembe, Wanging’ombe, Makete, Ludewa na Makambako yamekwenda Chadema.
Mkoa wa Rukwa
Jimbo la Mkasi Kusini, Kwela, Mkasi Kaskazini, Sumbawanga Mjini na Kalambo ni Chadema.
Mkoa wa Tanga
Handeni Mjini, Handeni Vijijini, Pangani, Tanga Mjini, Bumbuli,
Mlalo, Lushoto na Mkinga ambapo Korogwe, Muheza, Kilindi na Korogwe
Vijijini ni Chadema.
Mkoa wa Kilimanjaro
Jimbo la Rombo, Same Magharibi, Same Mashariki, Moshi Vijijini, Siha, Moshi Mjini na Hai ni Chadema huku Vunjo ikienda kwa NCCR.
Mkoa wa Arusha
Jimbo la Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Arusha Mjini, Longido, Monduli, Karatu na Ngorongoro ni Chadema.
Mkoa wa Manyara
Jimbo la Simanjiro, Mbulu Vijijini, Hanang, Babati Mjini, Babati Vijijini, Kiteto na Mbulu Mjini ni Chadema.
Mkoa wa Pwani
Jimbo la Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji Utete, Mafia, Rufiji na
Kibiti ambapo Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Chalinze ni Chadema.
Mkoa wa Morogoro
Jimbo la Kilosa na Morogoro Kusini Mashariki (CUF) ambapo Mikumi,
Morogoro Kusini, Kilombero, Mlimba, Mvomero, Ulanga Magharibi, Ulanga
Mashariki na Morogoro Mjini ni Chadema.
Mkoa wa Dodoma
Jimbo la Kondoa Mjini, Kondoa Vijijini na Chema ni CUF; Jimbo la
Kibakwe na Mtera ni NCCR-Mgeuzi huku Jimbo la Kogwa, Dodoma Mjini, Bahi
na Chilonwa yakiwa ni ya Chadema.
Mkoa wa Singida
Jimbo la Iramba Magharibi, Iramba Mashariki, Singida Kaskazini,
Singida Mashariki, Singida Magharibi, Manyoni Magharibi na Manyoni
Mashariki ni Chadema.
Mkoa wa Tabora
Jimbo la Bukene, Nzega Vijijini, Igalula, Tabora Kaskazini, Kaliua na
Tabora Mjini ni CUF ambapo Jimbo la Nzega Mjini, Igunga, Urambo,
Ulyankulu, Sikonge na Manonga ni Chadema.
Mkoa wa Katavi
Jimbo la Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Katavi, Nsimbo na Kavuu ni ya Chadema.
Mkoa wa Kigoma
Buyungu, Mhambwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini,
Manyovu (NCCR-Mageuzi) na Kigoma Kaskazini pia Kigoma Mjini ni Chadema.
Mkoa wa Ruvuma
Jimbo la Tunduru Kaskazini, Namtumbo na Tunduru Kusini ni CUF ambapo
Mbiga Mjini ni NCCR-Mageuzi. Jimbo la Madaba, Songea Mjini, Mbinga
Mashariki/Mbinga, Mbinga Maghribi/Nyasa na Peramilo ni Chadema.
Mkoa wa Mtwara
Jimbo la Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba, Mtwara Vijijini,
Nanyamba na Nanyumbu ni CUF ambapo Jimbo la Lulindi, Masasi na Ndanda ni
NLD.
Mkoa wa Lindi
Jimbo la Mtama, Kilwa Kaskazini, Kilwa Kusini, Lindi Mjini, Ruangwa, Nachingwea, Liwale na Mchinga ni CUF.
Post a Comment