MTABIRI
maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ameibuka na kusema kwamba utabiri
aliowahi kuutoa kwamba kuna mgombea urais atafariki, bado upo palepale.
Maalim
Hassan alisema kuugua ghafla kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ni dalili tu za ukamilifu wa utabiri
wake lakini suala la mgombea urais kudondoka na kufa akiwa jukwaani
akifanya kampeni linakuja.
“Kuugua
kwa Mbowe hakujatimiza utabiri kama ulivyosema ila hizo ni dalili tu
lakini kuna mgombea atadondoka jukwaani akifanya kampeni na atakufa
lakini haioneshi ni wa chama gani na hii ni kutokana tu na mwaka huu
ulivyoanza kinyota,” alisema mtabiri huyo.
Mwaka
huu mwanzoni mtabiri huyo alitoa utabiri uliyoonyesha kwamba kutakuwa
na kifo cha mgombea urais pamoja na mambo mengine ikiwemo kuibuka kwa
magonjwa ya kushangaza
~Mpekuzi blog
Post a Comment