Chamangeni Zulu akiuguza majeraha yake hospitalini.
Waswahili wanasema akili za kuambiwa changanya na zako wakimaanisha si kila kitu unachoambiwa ukifuate isipokuwa kichuje na ndipo ufanye maamuzi
Kuna watu wanaopenda kwenda kwa waganga na kufuata kila wanachoambiwa bila kufikiria vizuri madhara yake na hii imejitokeza kwa mkazi wa nchini Zambia.
Huyo kijana Chamangeni Zulu kutokea Malawi amejikuta akiliwa sehemu zake za siri na fisi pamoja na kukosa vidole vitatu.
Zulu alitaka utajiri na akaenda kwa mganga ambaye alimweleza kuwa ili aweze kuwa tajiri anatakiwa kupoteza sehemu ya viungo vya mwili wake.
Kwa sasa Zulu yupo kwenye hospitali Kuu ya Chipata nchini Zambia karibu na mpaka wa Malawi.
Zulu alimwachia mwenyewe fisi amle sehemu zake za siri.
Zulu ameliambia gazeti la The Times kuwa "Nilikutana na wafanyabiashara walionieleza kuwa njia nzuri ya kuwa tajiri ni kutoa sehemu ya viungo vyangu vya mwili".
Anasema majira ya saa 10 alfajiri wiki mbili zilizopita alikwenda msituni kwa upande wa Zambia.
"Nilielekezwa niwe uchi na nilipofika huko alikuja fisi akaanza kunila vidole vyangu na mara akala sehemu zangu za siri,"anasimulia.
Zulu anasema mganga aliyempa maelekezo hayo hakumweleza wazi kuwa sehemu zake za siri zitapotea zote.
Licha ya tukio hilo la kumuumiza, Zulu anaamini atakuwa tajiri baada ya nyeti zake kuliwa.
"Hata kama nimepoteza sehemu muhimu za mwili wangu bado naamini nitakuwa tajiri,"anasema.
Raia huyo wa Malawi amekuwa akiishi na kufanya kazi Zambia kwa miezi minne sasa.
Uongozi wa Hospitali ya Chipata umesema Zulu alifikishwa hospitalini hapo na maofisa polisi na hali yake inaendelea vizuri.
Mwaka 2012 umbali wa maili 50 katika eneo la Chadiza mwanaume mmoja alivamiwa na mnyama wakati akienda kujisaidia kwenye bustani yake.
Mwanaume huyo, Isaac Mwale(42) alisema alimuona mnyama mweusi anayefanana na mbwa na kumvamia kabla ya kuondoka na mguu wake.
Baada ya shambulio hilo, wanakijiji walishitaki kwenye Mamlaka ya Wanyamapori ya Zambia kupunguza idadi ya fisi katika eneo hilo.
Post a Comment