Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Jux ampamba Joh Makini kwa kazi zake

Msanii Juma Jux ambaye ni mshindi wa tuzo ya wimbo bora wa RnB (2014) katika tuzo za Kilimanjaro Music Award ameonyesha mapenzi yake na kukubali kiwango cha rapa kutoka katika kundi la Weusi, Joh Makini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkali huyo wa RnB amesema wakati anaanza kufanya kazi ya muziki alikuwa anavutiwa sana na kazi zake na tangu amemfahamu anakiri wazi kuwa hajawahi kuona ameshuka katika viwango vyake vya muziki bali anazidi kufanya poa siku hadi siku na kuzidi kuwa bora zaidi.

Jux amesema kutokana na Joh makini kufanya kazi bora kila siku maanimi kuwa ndio maana watu walimpa jina la Mwamba wa Kaskazini.
A photo posted by juma_jux (@juma_jux) on

 "Kipindi naanza muziki nilikuwa namsikia tu Joh Makini na nakuvutiwa sana na kazi zake. Na tangu namfahamu mpaka sasa hajawahi kushuka ni kupanda tu kwenye sanaa, I guess that's why they call him Mwamba," alisema Jux.

Wakali hao wawili wamekutana katika kazi moja ambayo inakwenda kwa jina la 'Nakutafuta' Looking for you' ambayo ni kazi ya Jux akimshirikisha Joh Makini na video ya wimbo huo umefanyika Afrika Kusini na mwongozaji video Justin Campos.

Jux anasema alishukuru sana baada ya mkali Joh Makini alipokubaliana na ombi lake la kufanya kazi pamoja na kuweza kuweka mistari mikali katika wimbo huo ambao kwa mara ya kwanza umeaanza kuonekana katika vituo vya Luninga vya kimataifa.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top