Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CCM Wakanusha Habari Iliyoenea Kuwa Mgombea Wake, Dr John Magufuli Ameahidi Kugawa Laptop Kwa Walimu Wote Nchini

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.

Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.

Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho.

 
" Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23 mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzihiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.
Nape Nnauye akionesha kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo imepitishwa jana Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama hicho uliofanyika jana mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23,mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo wa CCM mapema leo jijini Dar.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top