Mwaka 1985 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988.
Mwaka 1989 - 1995 alifanya kazi katika kiwanda cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.) akiwa mkemia na wakati huohuo alianza masomo ya shahada ya uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza, kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisoma kati ya mwaka 1991 na 1994.
Magufuli aliendelea na elimu ya juu zaidi kwa maana ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia kuanzia mwaka 2000 hadi 2009 ambayo aliihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa mhitimu wa shahada ya udaktari. Dk Magufuli ana mke, watoto na familia imara.
Jambo jingine linaloweza kumvusha Magufuli ni msimamo. Yeye ni kiongozi mwenye misimamo isiyotia shaka. Hajui kuuma maneno lakini anajua nini anachokisimamia. Watendaji wa Wizara ya Miundombinu wanasema ni vigumu kumyumbisha Magufuli katika jambo ambalo anaona hilo ndiyo njia, lazima mlitekeleze kwanza. Tabia ya namna hiyo alikuwa nayo Mwalimu Julius Nyerere, kwamba akishaamua jambo fulani na kama anajua njia yake, humtoi relini.
Post a Comment