Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Lowassa Awaweka Ukawa Njia Panda! Chama Chagawanyika Wengine Wamtaka Lowassa Wengine Wamkataa....

Ojuku Abraham
SINTOFAHAMU! Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD sasa upo njia panda kuhusu ujio wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anayesemwa kutaka kutimka kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
slaa

Habari kutoka ndani ya vyama hivyo zinasema, tangu kukatwa kwa Lowassa katika kuwania kwake kuteuliwa kuwa mgombea urais, kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa watu mbalimbali, wanaotaka kada huyo wa chama tawala anayetajwa kuwa na wafuasi wengi ajiunge na Chadema, ili awanie nafasi hiyo kwa tiketi ya Ukawa.


“Kuna vikao vingi ndani ya vyama hivyo kiasi kwamba wameshindwa kumtaja mgombea wao ili kusubiri kwanza wajue hatima ya Lowassa. Inadaiwa kuwa Chadema imegawanyika, kwani baadhi ya vigogo wanamtaka kada huyo wa CCM na wengine wanapinga, CUF wanamtaka hata sasa hivi. Ninachoweza kukuambia ni kwamba ndani ya Ukawa, hali ni tete, haieleweki,” kilisema chanzo chetu kilichopo ndani ya umoja huo.

Licha ya viongozi wakuu, chanzo hicho kilidai kuwa hata makada wa kawaida wa Chadema, chama kinachodaiwa kuwa ndiyo lengo la Lowassa, wamegawanyika, kwani wapo wanaomuona kama mwenye mtaji mkubwa kisiasa, huku wengine wakimuona ni doa litakalowapa tabu kuliondoa.

Shinikizo la Lowassa linatokana na ukweli kuwa kwa muda mfupi tangu jina lake liondolewe na Kamati ya Maadili ya CCM kiasi cha kutowasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu, makundi mbalimbali ya makada wamejiengua kutoka chama tawala na kujiunga na Chadema, wakiwemo zaidi ya madiwani kumi na nne na wenye viti wa vijiji wilayani Monduli.
Akizungumzia kuhusu uwezekano wa Lowassa kujiunga na Chadema, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema kilichopo ni uvumi tu ambao hata wao wamekuwa wakiusikia hivyo hana cha kuzungumzia.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top