Diamond kabla ya mafanikio.
Kampuni ya Coca-Cola Afrika ya Kati, Mashariki na Magharibi imezindua kampeni mahsusi ijulikanayo kama ‘Sababu Bilioni za Kuamini’ inayolenga kuwahamasisha vijana wa Kitanzania kujiamini pindi wanapopita katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kimaisha kabla ya kutimiza ndoto zao. Kampeni hiyo ya miezi mitatu itaendeshwa nchi nzima.
Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ni miongoni mwa vijana wanaotolewa mfano katika dhana hii. Alitengeneza single zaidi ya 20 kabla ya kufanikiwa na hatimaye kufikia katika mafanikio makubwa aliyonayo sasa
Mwaka 2007 Diamond alifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuuza mitumba, kufanya kazi katika vituo vya kujaza mafuta pamoja na kupiga picha mitaani ili aweze kupata fedha zilizohitajika studio.
Diamond Platnumz
Hata hivyo, hakukata tamaa na ni kutokana na moyo wake huo wa kutokubali kushindwa kwa urahisi ameweza kufanikiwa na kuwa miongoni mwa nyota wachache wa muziki anayetamba aliye kijana tajiri mkubwa kwa sasa hapa nchini.
“Kupitia kampeni hii, Coca-Cola itaweza kuwaletea simulizi zaidi juu ya mafanikio ya watu ambao hawakukata tamaa licha ya kutofanikiwa mara kadhaa katika safari zao za kuelekea kwenye mafanikio. Sababu zilizowafanya wasikate tamaa ni kutokana na imani yao kuwa kuna siku ambayo wangekuja kufanikiwa. Na hicho ndicho tunachotaka vijana wa Kitanzania waweze kuiga. Wawe na moyo wa kutokata tama licha ya kukumbana na changamoto nyingi katika safari yao kuelekea katika mafanikio,” Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka.
Coca-Cola imewekeza katika programu ya soka kwa vijana ijulikanayo kama Copa Coca-Cola ambapo vipaji vya wachezaji nyota kama vile Thomas Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya nchini Congo na mfungaji bora wa ligi kuu nchini Simon Msuva anaechezea Yanga vimeweza kuibuliwa na Copa Coca-Cola. Vile vile Coca-Cola inasaidiia kuinua wanamuziki wa Tanzania kupitia programu ya Coke Studio.
Simon Msuva
Thomas Ulimwengu
Katika kipindi hicho cha kampeni, Kampuni ya Coca-Cola itakutana na kuwafikia kwa karibu zaidi vijana shuleni na maeneo mengine wanakoishi ili kuwawezesha kutambua uwezo walionao katika kufanikisha maisha yao. Itawawezesha kusimulia hali halisi ya maisha yao na ndoto wanazokusudia kuzifanikisha katika maisha. “Coca- Cola inatumia kampeni hii kuwahamasisha na kuwajengea uwezo ninyi vijana wa Kitanzania muweze kujiamini kutokana na uwezo mlionao katika dunia tuliyomo ambayo mambo yasiyo na uhakika yanazidi kuongezeka,” alisema Njowoka. Kampeni ya Sababu Bilioni za Kuamini (Billion Reasons to Believe- BRTB) inalenga kuwafanya vijana wajiamini na kutoyumba katika kuzifikia ndoto walizojiwekea licha ya mara kadhaa kukumbana na changamoto zilizowafanya kutofanikiwa kila walipojaribu katika hatua za awali.
Sababu Bilioni za Kuamini ni kampeni inayoendeshwa kwa njia mbalimbali ambazo ni pamoja na TV, radio, matumizi ya njia za kidigitali na matangazo ya nje ikiwa ni pamoja na shughuli za maonyesho ili kuwezesha ushiriki wa watu wengi nchi nzima.
Post a Comment