Wasichana wengi siku hizi wamekua na tabia ya kupenda vitu vya anasa hali inayopelekea sisi wanaume kuwaogopa kama ukoma.Mfano kutaka kufanyiwa shopping za bei mbaya,kumiliki simu za gharama zinazoanzia milioni moja na kuendelea,kupenda kuwa na mwanaume mwenye mshahara unaoanzia milioni tatu kwa mwezi na kuendelea n.k
Hali hii inasababisha hata sisi wenye kipata cha laki saba kushuka chini tuwaogope kwa kuamimini kwamba hatuna uwezo wa kukidhi mahitaji yenu hatimaye mnajikuta mnazeekea nyumbani kutaamakitaamaki miaka 45 hii hapa ambapo ndo kipindi cha menopause kwa mwanamke yeyote.
Msipende mteremko sababu hata huyo mwenye magari,majumba na kipato kikubwa hujui ametumia njia gani mpaka kupata hivyo vitu.Starehe hazina mwisho hivyo unapobweteka na starehe fahamu kwamba fainali uzeeni muda ndio refa.
Aliesikia na asikie na alieamua kupuuzia na apuuzie
Post a Comment