Alikiba na Jokate wanadaiwa kuwa na uhusiano. Wema amekuwa upande wa
Kiba tangu kuachana na Diamond na wengi wamekuwa wakikichukulia kama ni
kisasi.
Baada ya ushindi huo warembo hao walitumia Instagram kutoa pongezi zao.
“Hongera sana cherie @officialalikiba kwa kujishindia tuzo sita jana
usiku kwenye kiba Tanzania music awards (KTMA) sorry Kilimanjaro
Tanzania music awards 2015. Teh teh the,” aliandika Jokate.
“Ni kitu cha kumshukuru Mungu ulikaa kimya miaka 3 ila ukarudi na wimbo
mmoja ukatuteka tena. Kusema ukweli tukiachilia mbali ushabiki ‘mwana’
ulituliza akili na ukafanya vizuri sana nchini. Mashabiki wanakupenda.
Sana. Mpole hivi, mcheshi, mstaarabu. Na unajua mziki. Tunakuombea sasa
hii iwe motisha ya wewe kufika mbali zaidi. Ndio kwanza safari imeanza.
Uzuri unaomba mungu so najua hata kutupa. Ila kaza mwana we kazaaa!!! We
are behind you,” aliongeza.
Naye Wema aliandika: Nilitaka zote saba ila hata 6 pia sio mbaya…. #KingKiba…. Umetisha.”
Jokate pia amepost picha akiwa na Wema na kuandika: It’s a beautiful and
powerful thing when strong girls come together. emojiemojiemoji️. With
The Sweetheart @wemasepetu.”
Post a Comment