Mwamamuziki, Jennifer Lopez ‘J.Lo akitumbuiza pamoja na dancers wake. Rabat, Morocco
WAZIRI wa Mawasiliano wa Morocco, Mustapha Khalfi, amejikuta katika wakati mgumu kufuatia kufanyika kwa shoo ya mwamamuziki, Jennifer Lopez ‘J.Lo, ambaye alivaa mavazi yaliyoacha nje asilimia kubwa ya maungo yake pamoja na dancers wake.
Shoo hiyo ilifanyika Mei 29, mwaka huu katika Tamasha la Mawazine lililofanyika huko Rabat na kuonyeshwa moja kwa moja na Runinga ya 2M ya nchini humo.
Hata hivyo, sasa suala hilo linapamba moto kufuatia wanasiasa wa Dini ya Kiislam kuja juu na kumtaka waziri huyo ajiuzulu, kwani shoo hiyo ilikosa adabu na kudhalilisha, hata hivyo waziri huyo amegoma kuachia ngazi.Staa mwingine aliyepafomu katika tamasha hilo ni Pharrell Williams ambaye yeye hakuzungumziwa jambo lolote baya.
Post a Comment