Baada ya kupotea kwa muda mrefu, msanii wa filamu ambaye pia ni Miss Ruvuma 2007, Neema Chande ameibuka akiwa na mimba kubwa huku kukiwa na usiri juu ya mhusika wa tumbo hilo.
Msanii wa filamu ambaye pia ni Miss Ruvuma 2007, Neema Chande.
Neema hivi karibuni alikimbilia nchini India kusaka maisha na
alipozungumza na mwandishi wetu juzi kwa njia ya simu alisema, watu
wajue tu kwamba ana mimba aliyopewa na Muafrika mwenzake na anatarajia
kujifungua ‘soon’.“Nimefurahi sana kwani siku zote nilikuwa nikitamani maisha haya ya kulea tumbo na ‘soon’ nitarudi Tanzania kwa ajili ya kumuweka wazi baba kijacho kwani tuna mipango mizuri ya maisha,” alisema Neema.
Post a Comment