Gladness Mallya na Hamida Hassan
MAKUBWA! Yule bwana ambaye ni kigogo serikalini (jina tunalihifadhi kwa sasa) aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu na kumwagana naye, taarifa zimevuja kwamba kwa sasa amemnasa mwigizaji Ester Kiama ambaye anampa jeuri ya kuishi mjini. Kwa mujibu wa chanzo makini, kigogo huyo ambaye anamiliki maduka kadhaa ndani ya Mlimani City, ndiye anayempa jeuri Ester kwa kumfungulia biashara mbalimbali na fedha kwa ajili ya kutengeneza filamu zake mwenyewe licha ya kuwa mrembo huyo naye ana biashara zake nyingine ikiwemo ya kuuza magari.
“Ester ana maisha mazuri mno na yote hayo anafanyiwa na aliyekuwa bwana wa Wema, ndiyo maana unamuona sasa hivi yuko matawi ya juu kushinda wasanii wenzake wa kike,” kilidai chanzo chetu.
Baada ya kuzipata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Ester, mambo yalikuwa hivi:
Ester KiamaIjumaa: Hongera maana tunasikia sasa hivi umepata bwana mwenye nazo.
Ester: Mh! Mmeanza mambo yenu.
Ijumaa: Mambo gani wakati tumeambiwa sasa uko na yule kigogo aliyekuwa akimpa jeuri Wema?
Ester: Hahaa, nani kawaletea umbeya huo?
Ijumaa: Sisi tunapewa habari kutoka kwa watu wanaokuona naye, wewe tuambie umeamua kutulia hapo kwa sasa? Au huna uhusiano naye?
Ester: Jamani haya mambo ya uhusiano ni maisha yangu binafsi, please naomba mniache, siku zote mimi siyo mtu wa kuanika maisha yangu binafsi.”
Ijumaa: Oke tunashukuru.
Post a Comment