Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na
wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali
unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa
Rufaa (Mst.) Damian Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa
mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria
ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia
kuanza hivi karibuni.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani
unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na kampeni za Uchaguzi kwa
wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.
Halikadhalika
siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015
kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Mpekuzi blog
Post a Comment