London,England
ARSENAL leo Jumamosi inacheza fainali yake ya 19 ya
Kombe la FA huku ikiwa na rekodi ya kuwa kinara wa kutwaa mara nyingi
taji hilo sambamba na Manchester United ikiwa imetwaa mara 11.Klabu hii
ya London, kwenye Uwanja wa Wembley inacheza na Aston Villa ya jijini
Birmingham.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Sanchez.
Hadi inafikia hatua ya kucheza fainali, Arsenal iliitoa Reading
katika nusu fainali wakati Aston Villa iliitoa Liverpool. Timu zote
zilishinda mabao 2-1.Ikiwa chini ya Kocha Arsene Wenger, Arsenal inataka kuandika rekodi mpya kwa kutwaa mara ya 12 taji hilo na kuiacha Man United ambayo imetwaa mara 11.Arsenal inaingia uwanjani ikiwa ni bingwa mtetezi kwani msimu uliopita ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Hull City mabao 3-2, hivyo kuna kitu ambacho Wenger atataka kukifanya ili kuandika rekodi mpya.
Rekodi zinaweka wazi kwamba, mara ya mwisho Arsenal kutinga fainali ya Kombe la FA na kufungwa ilikuwa mwaka 2001, wakati ilitwaa taji hili kwa mara ya kwanza mwaka 1930 (kumbuka Simba na Yanga zilikuwa bado hazijaanzishwa).
Aston Villa yenyewe imetwaa ubingwa wa Kombe la FA mara saba huku ikicheza fainali mara kumi na kwa mara ya kwanza ilitwaa ubingwa wa michuano hii mwaka 1887 na mara ya mwisho kucheza fainali ilikuwa mwaka 2000 na ikapoteza.
Mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke.
Mara ya mwisho kwa Aston Villa kutwaa ubingwa wa Kombe la FA ni mwaka
1957. Hata hivyo, wakati huu ikiwa chini ya Kocha Tim Sherwood sasa
itajitahidi kuweza kutwaa ubingwa huo.Nyota kama Shay Given, Joe Bennett, Tom Cleverley, Scott Sinclair, Gabriel Agbonlahor, Joe Cole, Fabian Delph, Darren Bent, Charles N’Zogbia na Christian Benteke, watapambana kuhakikisha Aston Villa inatwaa ubingwa.
Tofauti na Aston Villa iliyoshika nafasi ya 17 katika msimu uliopita wa Ligi Kuu England, Arsenal iliyoshika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo, katika fainali hii inaweza kuwakosa nyota wake Theo Walcott, Jack Wilshere na Danny Welbeck ambao ni majeruhi.
Walcott alirejea uwanjani kwa kasi katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu England dhidi ya West Brom na kufunga mabao matatu ‘hat trick’ na wengi walidhani angecheza leo lakini kuna shaka ya kujumuhishwa kikosini. Wilshere, bado anaonekana hayupo vizuri kwani tatizo lake la kifundo cha mguu limechangia kushusha kidogo kiwango chake hivyo kuna shaka ya yeye kucheza leo
Kombe la FA.
Kuhusu wachezaji hao, Wenger anasema: “Sijui nani atakuwa fiti siku
hiyo hivyo siwezi kujua nani atacheza au nani hachezi, isipokuwa jambo
muhimu kwetu ni kutwaa taji hili siyo kujali nani atakaa benchi na nani
atacheza.”Kuhusu Welbeck ambaye hajacheza tangu aumie katika sare ya bila mabao na Chelsea Aprili 26, mwaka huu na Wenger amesema; “Hatakuwepo, nilijiandaa kwa hilo. Hajafanya mazoezi tangu Ijumaa iliyopita, hivyo nilijua atakosekana katika fainali ya FA.”
Post a Comment