BAADA ya kuzagaa kwa habari kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ‘kutembea’ na mrembo wa Bongo Movies, Kajala Masanja, mheshimiwa huyo ameibuka na kuzungumzia tuhuma hizo kuwa hazina ukweli wowote zaidi ya kutaka kumchafua katika uongozi wake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Mapema wiki hii, mitandao mbalimbali ya kijamii ilimtuhumu mheshimiwa
huyo kwamba ana uhusiano na muigizaji huyo kwa kudai amekuwa akionekana
naye mara kwa mara.Makonda ambaye ameonesha uchapakazi uliotukuka baada
ya kuteuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa wilaya hiyo mapema
mwaka huu, ameweka bayana kuwa kwa muda mrefu kuna watu wenye nia mbaya
ambao wanaendesha kampeni ya kumchafua.“Ni muda mrefu tu, walianza kipindi kile wakati wa Bunge la Katiba nilipokwenda Bungeni na mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, wakasema natembea naye, wakanyamaza. Sasa wamehamia kwa Kajala baada ya kufanya naye kazi.
Mrembo wa Bongo Movies, Kajala Masanja.
“Hakuna ukweli wowote wanatungatunga tu mambo, watakuwa na sababu zao
kwa sababu mtu kama Kajala, maneno yameibuka baada ya kufanya naye
project ya kutafuta vipaji vya wasanii.“Nimeshirikiana na wasanii wengi
wa kiume katika project hiyo lakini kwa kuwa wameona mwanamke ni Kajala
peke yake, wanasema vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Najua kuna
wengine wanaoeneza haya mambo wanatumika kisiasa lakini mimi sijali.“Waniache nifanye kazi, najitoa kwa wasanii kwa nia njema ya kutafuta wasanii ambao baadaye wataweza kujitegemea kwani sanaa ni ajira, kamwe hawawezi kurudisha nyuma juhudi zangu,” alisema Makonda ambaye amejiwekea utaratibu wa kukutana na wakazi wake kila Ijumaa kutatua migogoro ya ardhi.
GLOBAL NEWS
Post a Comment