Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Video: Young Dee Ft Ben Pol - 'Do It'

Watch the brand new video "DO IT" by Tanzanian Rapper Young Dee Feat. Ben pol.

Amber Rose na swahiba wake Blac Chayna kuja na TV Show ya pamoja

Amber Rose mwishowe aamua kuja na TV Show yake itakayo muonyesha maisha yake ya kila siku, Na swahiba wake Blac Chyna anaonekana kupendelea kujiunga kwenye project hiyo.
Kwanzia mwanzoni mwa mwaka huu kumekuwa na tetesi za model huyu Amber Rose ambaye alishawahi kuwa na Kanye West kimapenzi na mastaa wengine hadi kufikia kuolewa na Wiz Khalifa na kubahatika kupata naye mtoto mmoja kabla ya ndoa yao kuvunjia kuwa atakuja na TV Show inayo muonyesha maisha yake ya kila siku.
Mwezi wa May, Amber aliposti picha inayoonyesha eneo kama studio ya television yenye tv screens kubwa zinazo onyesha jina lake.
Nick Cannon, ambaye ni rafiki wa karibu wa Amber Rose alitakiwa kuonekana mtu wa karibu kumsaidia Rose kwenye project hii, Lakini hadi sasa hajasikika akiliongelea suala hilo kwanzia tetesi zivume.

Hataivyo mtandao wa TMZ umehabarisha kuwa project hiyo bado inaendelea na Rose muda ataanza kuonesha TV Show yake inayo tarajiwa kuwa na watazamaji wengi kama ilivyo ya Kim Kardashia huku swahiba wake Blac Chyna ambaye alisha wahi kuwa na Tyga atakuwa co-star.

Ni zamu ya Nay wa Mitego kaonesha kumsupport Mgombea wa Urais 2015…

Mwaka huu ni headlines za Uchaguzi 2015 tumeona baadhi ya wasanii wameonesha kutoa support kwenye kipindi hiki kwa wagombea Urais wawili ambao ni John Pombe Magufuli atakaegombea CCM na Edward Lowassa kupitia CHADEMA.

Miongoni mwa wasanii waliojitokeza na kutangaza rasmi kumsupport mgombea Urais kupitia CCM, Dkt.John Pombe Magufuli, kuna Wema Sepetu, Batuli, Snura, Linex, Steve Nyerere, Diamond Platnumz, Shetta, Barnaba,Bushoke, Kysher, Wastara na wengineo huku mwigizaji Aunty Ezekiel na Jackline Wolper wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni zamu ya Nay wa Mitego.
Nay wa Mitego anamsupport Edward Lowassa kayaandika haya….>>>>Huwezi zuia Mvua ikiamua kunyesha inanyesha tu! Tuna Imani na Lowassa. Ccm wote bado wana Imani na Lowassa hata Kura za Urais ni kwa Lowassa.Nilikua sipost chochote coz Nilikua nataka nisikie CCM labda wana jipya juu ya sera yao mwaka huu coz upinzani umekua mkali, wangenishawishi kidogo. Dooh ndo wameongeza uozo mara dufu.Watanzania wameamka si kwa uongo ule wa jana ���� Milioni Hamsini kila Kijiji. Tanzania ina vijiji vingapi? Piga Hesabu ya haraka kadilia, si chini ya bilioni 600 na zaidi.Watanzania sio mazoba kiasi hicho tumeshtuaa…Hamjajipanga mwaka huu mmetukosa..#Mabadiliko2015

ZARI BOSS LADY AMPA DIAMOND KAZI YA ZIADA ALIBADILI JUMBA LAKE LIKAE KISASA ZAIDI



Picha: Inawezekana huyu ndiye mpenzi mpya wa Chris Brown, Ni baada ya kuonekana naye akiwa na mtoto wake Royalty

Chris Brown, Mama yake na mpenzi wake mpya walionekana wakiwa pamoja juzi August 25, 2015 kwenye mitaa ya NYC. Hizi ni picha zinazo onyesha walivyo kuwa wakizunguka eneo moja huko Ney York City na pia nimekuwekea picha za mrembo huyo akiwa mwenyewe.






Joh Makini amfanya Diamond Platnumz aongelea haya juu ya Freemason

Idadi ya wasanii wa Tanzania wanaotuwakilisha kimataifa inazidi kuongezeka, pongezi kwa WEUSI kwa kuamua kujitoa kwa dhati na matunda ya jitihada zao yanaonekana.
Msanii anayeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania nje ya mipaka, Diamond Platnumz amefurahishwa na juhudi za Weusi katika kujitangaza kimataifa, ukizingatia ndio wasanii wa Hip Hop ambao nyimbo zao zimeanza kupewa nafasi kwenye runinga na radio za kimataifa zikiwemo Trace Urban na MTV Base.

Hayo hayakuja hivi hivi, mpaka pale Joh makini na wenzake kwa juhudi zao binafsi walipoamua kuwekeza na kwenda kushoot video ya ‘Nusu Nusu’ Afrika Kusini, na matokeo tayari tumeanza kuyashuhudia.

Hit maker wa ‘Nana’ amempongeza Joh Makini na Weusi ambao wamekamilisha kushoot video 2 ikiwemo ile ya collabo yao na rapper AKA wa Afrika Kusini.

Diamond ndiye aliyemleta AKA kwenye Zari All White Party jijini Dar mwezi May mwaka huu, na baada ya AKA kutua ndio Joh alipata nafasi ya kurekodi naye wimbo. Hivyo kwa sehemu kubwa pia Diamond amehusika katika kufanikisha collabo hiyo ambayo soon tutaanza kuiona katika runinga.

Kupitia Instagram hiki ndicho Diamond amekiandika kuhusu Weusi na harakati zao;
“Halaf kweli kesho na Kesho kutwa mtu anakuja anasema Ooh flani freemason ooh mara flani Sjui Anabebwa, ooh sjui Anaroga wakati mtu anaHaso na kujituma 24/7 kila mtu anaona…. mi nakuheshim sana @joh_makini na Team yako nzima ya WEUSI kwa juhudi na Harakati zenu za kilasiku mnazozizidisha…Mwenyez Mungu Aendelee kuwasmamia na Kuwabariki.”

Picha na Video: Waandishi 2 wauawa wakiwa hewani 'Live' Marekani (Samahani kwa picha na video hizi)

Waandishi wawili wa habari wamepigwa risasi katika jimbo la Marekani la Virginia wakati wakifanya mahojiano ya moja kwa moja ya runinga.
Kanda ya video inaonyesha mwandishi wa habari wa kike akimtania mgeni aliyekua akimuhoji kabla ya risasi kufyatuliwa mara nane.
Mwandishi huyo anaonekana akiruka na kamera kuanguka sakafuni huku mwanamume aliyevalia nguo nyeusi na kubeba bunduki akipita karibu.

Kituo kilichoajiri waandishi hao cha WDBJ kinasema mwandishi huyo wa habari Alison Parker na mpiga picha Adam Ward walikufa katika tukio hilo .
Polisi wanasema mshukiwa hajulikani aliko.



MAGUFULI AFANYA MKUTANO WA KIHISTORIA MKOANI MBEYA

 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia c\Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyia Oktoba 25 mwaka huu.
Wananchi wakimsikiliza Magufuli
Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya
Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni

Tangazo la Wito chuo cha polisi moshi kwa wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2014 na JKT mwaka 2015 waliochaguliwa kujiunga na jeshi la Polisi.

JIONEE PICHA VIJANA WA LEO WANAVYOPENDA STAREHE BALAA











Magazeti 21 ya Tanzania August 27 2015, habari kubwa za udaku, michezo na hardnews

Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Alhamisi Agosti 27,2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa

. .


.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.
.
© Copyright 24hours
Back To Top